Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji haramu 54 waliofichwa kwenye magodoro wakamatwa (+picha)

WhatsApp Image 2021 06 17 At 18.03.53 1 660x400.jpeg Wahamiaji haramu 54 waliofichwa kwenye magodoro wakamatwa (+picha)

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Pwani imewakamata wahamiaji haramu 54 kutoka Ethiopia ambao waliokuwa wanasafirishwa katika lori ya mizigo lililobeba magodoro kutoka Bagamoyo na kukamatiwa Msola Chalinze Mkoa wa Pwani.

Hayo ameyaeleza Afisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Omary Hassani mara baada ya kukamta lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 191 AYD lililokua linaelekea Tunduma Mkoa wa Songwe huku likiwa limewaficha Wahamiaji haramu katikati ya magodoro ambayo yaliwekwa mlangoni kuwaficha wasionekane na wanamshikilia dereva wa lori hilo na wakala wa kusafirisha watu hao.

Aidha Kamishna Msaidizi Omary amesema kufanikiwa kuwakamata Wahamiaji haramu hao ni ushirikiano baina ya idara ya uhamiaji Mkoa wa Pwani na Polisi Mkoa huo ambao wote wanaendesha operation za kuwatafuta watu hao kuwafikisha Mahakamani.





Chanzo: millardayo.com