Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wahamiaji haramu kumi na moja 11 raia wa nchini Rwanda na Burundi kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ameeleza kuwa wahamiaji hao walikamatwa mnamo Februari 7, 2022 majira ya saa 12:00 jioni katika kizuizi cha Polisi Chalangwa kilichopo Kata ya Chalangwa, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, wakiwa wanasafiri ndani ya gari lenye namba za usajili T.295 DBQ Basi mali ya Kampuni ya Prince Ahmed wakitokea Tabora kuelekea Mbeya.
Wahamiaji hao wakiwemo watoto wadogo sita [06] wafahamika kwa majina:-
1. AKULIMANA EMANUEL [40] 2. QUIZERA RACHEL [32] 3. AMANI HORESI [32], 4. TUYIZERE WELLORL [32] 5. MOSES RAPHAEL [20] 6. KWIZELA WILES, mwaka 1.5 7. BUMTUBWIMINO JEHOVANIS [14] 8. MIYOBYOSE JUSTIN [06] 9. ISHIMWE ALINE [15] 10. SHIMI ARENI [15] 11. WIZEMANA CRIMANTINE [15]
Watuhumiwa wanafanyiwa mahojiano na kisha watakabidhiwa idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.