Jeshi la Polisi limewakamatwa wahamiaji haramu 16 waliotoka nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Mei 5, 2022 amesema wahamiaji hao wamekamatwa katika matukio mawili tofauti.
Kamanda Kuzaga amesema katika tukio la kwanza wahamiaji haramu 13 wa Ethiopia walikamatwa katika kijiji cha Ngage kata ya Loibosoit wilayani Simanjiro.
Amesema raia hao 13 wa Ethiopia waliokuwa wamepakizwa katika gari ambapo dereva alitoroka na raia mmoja wa Ethiopia ambaye hakufahamika.
Akizungumzia wahamiaji haramu watatu wa Somalia amesema wamekamatwa katika wilaya ya Mbuu.
Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Beatrice Bwire amekiri kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu na kuwataka wananchi kuacha kufanya biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu kwani haifai watakamatwa.