Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji haramu 13 wakutwa wamekufa kando ya barabara

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wahamiaji haramu 13 kati ya 26 raia wa Ethiopia wamefariki dunia baada ya kutelekezwa na watu wasiojulikana eneo la Sangasanga katika barabara kuu ya Iringa - Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema tukio hilo liliripotiwa saa tisa alasiri kwa vyombo vya usalama ambavyo vilifika katika eneo la tukio na kuwakuta watu hao.

Mutafungwa alisema watumiaji wa barabara hiyo waliiona miili ya raia hao pembeni mwa barabara na kutoa taarifa kwa askari wa kikosi cha usalama barabara eneo la Sangasanga.

Kamanda huyo alisema kati ya raia hao yumo mtoto mwenye umri wa miaka minane na polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini gari lililofanya hivyo pamoja na wahusika wa tukio hilo.

Alisema miili hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na wenzao 13 wanapatiwa matibabu hospitalini hapo huku wanne afya zao zikiwa mbaya.

Mwananchi lililofika hospitalini hapo lilishuhudia walionusurika wakinywa uji akiwamo mtoto huyo.

Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Safina Mhindi aliwataka wananchi kutoa taarifa pale wanapobaini kuwapo kwa watu wanaowatilia shaka ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz