Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji haramu 12 kutoka Ethiopia wakamatwa Morogoro

64466 PIC+WAHAMIAJI

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro imewakamata wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia wote wakiwa hai wakitokea Jijini Tanga kwenda Afrika Kusini.

Wahamiaji hao walikuwa wakipita mkoani Morogoro, Mbeya hadi mpakani Tunduma kwa kile walichodai kwenda kutafuta maisha.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Jumatano Juni 26, 2019  Ofisa Uhamiaji mkoa wa Morogoro, Angela Shija amesema wahamiaji hao walikamatwa jana Jumanne kufuatia msako walioufanya kwa kushirikiana na Polisi katika kijiji cha Lugono wilaya ya Mvomero.

Shija amesema msako huo ulifanywa baada ya kupata taarifa za kiintelijensia za kuwepo kwa wahamiaji hao katika pori lililopo katika kijiji cha Lugono ambao walikuwa wamejificha kabla ya kuendelea na safari yao.

Amesema msako huo ulifanywa kwa kuweka mitego maeneo mbalimbali ya pori hilo la Lugono ambapo mbali ya kuwakamata wahamiaji hao pia walifanikiwa kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kusafirisha wahamiaji hao.

Shija amesema baada ya kumhoji mtu huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi alikiri kuhusika na usafirishaji wa wahamiaji hao na kwa sasa yuko mikononi mwa polisi kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani.

Pia Soma