Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji 74 wa Congo na Burundi wapandishwa kizimbani

Kongobu.jpeg Kundi la wahamiaji likiwa mahakamani leo

Thu, 31 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Burundi na Kongo wapatao 74, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikibaliwa na tuhuma za kuishi nchini bila kuwa na kibali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Godfrey Ngwijo imewataja baadhi ya washtakiwa hao kuwa ni, Hasafu Amos, Justine Sefana, Herisone Jackson, Richardmaftali Lucas, David Musa na Alex Silvester.

Washtakiwa hao wamefikishwa mbele ya Mahakimu wawili tofauti ambapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga inadaiwa washtakiwa 59 ambao ni Raia wa Burundi na Kongo DRC walikamatwa wakiishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali au nyaraka za kuwawezesha kufanya hivyo.

Washtakiwa 15 raia wa Burundi wamesomewa shtaka lao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Avodia Kyaruzi na kudaiwa kuwa, Machi 30, 2022 katika sehemu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam washtakiwa walikamatwa wakilishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali au nyaraka za kuwawezesha kuishi nchini humo.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 6, mwaka huu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live