Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji 55 wakamatwa Katavi

55 Ktv.png Wahamiaji hao wengi ni kutoka Burundi

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya uhamiaji mkoa wa Katavi limewabaini wahamiaji haramu 55 raia wa Burundi walioingia nchini bila ya kufuata taratibu na kuendelea kufanya kazi za vibarua mashambani, huku wengine wakifanya kazi katika machimbo ya dhahabu na baadhi yao wakiwaingiza watoto wao kusoma katika shule mbalimbali za msingi

Akitoa taarifa ya zoezi linaloendelea la msako, doria na ukaguzi Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Vicent Haule ambaye pia ni afisa uhamiaji wa mkoa wa katavi amesema zoezi hilo limefanyika katika maeneo ya ikola, ruhafwe na mpanda

Kati yao raia hao wa burundi saba bado wanachunguzwa, 30 watarudishwa burundi wakiwemo akina mama na watoto na 15 watafikishwa mahakamani

Bwana Haule pia amewataja raia watatu wa burundi waliotoroka katika makazi ya wakimbizi yaliyopo ya nyarugusu na nduta mkoani kigoma ambao amesema watarudishwa katika kambi hizo

Ameongeza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la uingizaji wa watoto kutoka Burundi kwa ajili ya kuja kupata elimu bure ambapo katika msako huu wamekamata wanafunzi katika shule mbalimbali za msingi

Aidha ameonya juu ya tabia ya kukaribisha raia wa kigeni kwa ajili ya vibarua mbalimbali kama kutunza mifugo na mashamba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live