Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji 13 wadakwa Mwanza

41646 Mwanzapic Wahamiaji 13 wadakwa Mwanza

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewakamata watu 13 wanaodaiwa kuingia nchini kinyume na taratibu.

Watu hao wanaodaiwa kuwa raia wa Ethiopia wamekamatwa leo Jumatano Februari 13, 2019 katika mtaa wa Nyaburogoya kata ya Nyegezi, jijini Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema watu hao umri wao ni kati ya miaka 21 hadi 27, hawafahamu lugha ya Kiswahili wala Kiingereza 

Amesema watano kati yao wamekutwa na hati ya kusafiria za Ethiopia zenye muhuri wa idara ya uhamiaji ya Kenya.

“Jitihada za kumtafuta mkalimani zinaendelea ili kufahamu walivyofika hapa nchini na nia yao ya kuwa Mwanza. Wote ni wanaume,” amesema.

Amesema wanashikiliwa na polisi katika kituo kikuu cha Nyamagana, akibainisha kuwa huenda wameletwa na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la David mkazi wa Nyegezi ambaye hajulikani alipo.

Amewataja kuwa ni; Detebo Degawa, Daniel Girma, Tadwas Addise, Teshome Tumebo,  Solomon Alficho, Rile Abat, Malkam Tadas, Ashanani Degara, Chufamo Baboro, Mamushi Hilemarian, Tekile Dilamo, Yose Manto na Dawit Abebe.

Amesema kwa sasa wanafanyiwa taratibu za kufikishwa idara ya uhamiaji kwa hatua nyingine za kisheria.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz