Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji 12 mbaroni

B9af9bf9031f2c664e59b9b43f70dc6c Wahamiaji 12 mbaroni

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAHAMIAJI haramu 12 wamekamatwa katika eneo la Mbande Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakiwa njiani kuelekea Afrika Kusinwa kupitia Zambia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema wahamiaji hao walikuwa wakibadilisha fedha kutoka dola za Maekani kwenda shilingi kwenye duka la kubadilisha fedha katika eneo hilo ndipo wakashtukiwa na kukamatwa.

Tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu mkoani Dodoma ni la pili ndani ya wiki moja baada ya wengine 29 kukamatwa katika eneo la Mtera, wilayani Mpwapwa wakielekea Makambako kwa lengo la kuvuka mpaka ili kwenda Afrika Kusini.

Muroto alisema katika kundi hilo la wahamiaji haramu waliokamatwa Mbande, Waethiopia ni 11 na mmoja ni Mkenya, walikuwa wakibadilisha fedha ili kupata fedha za Tanzania na kuvuka mpaka wakiwa pamoja na Mtanzania ambaye aliwatelekeza katika duka hilo.

Alisema kukamatwa kwa wahamiaji hao kunakuja kutokana na ulinzi uliopo mkoani Dodoma mkoa ambao ni makao makuu ya serikali na viongozi wa kitaifa wapo hapo.

Muruto alisema wahamiaji hao bado wanahojiwa na Uhamiaji na mahojiano yakikamilika watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo za kuingia nchini kinyume cha sheria na bila kuwa na vibali.

Muroto alisema kabla, wakati na hata baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu mkoa wa Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi na viongozi wa kitaifa wapo hapo, umeendelea kuwa salama na pia utaendelea kuwa salama hata wakati huu wa kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Chanzo: habarileo.co.tz