Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahalifu wanaotumia bodaboda kukiona

59892366a4036e344809201c4c841ab3 Wahalifu wanaotumia bodaboda kukiona

Tue, 1 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ameagiza kufanyika kwa operesheni za kuwasaka na kuwakamata wahalifu wanaotumia pikipiki kupora pamoja na wahalifu wanaojihusisha na uvunjaji na kuiba mali za wananchi.

IGP Sirro amesema hayo leo katika ukaguzi wa kushtukiza alioufanya kwenye kituo cha Polisi Stakishari, Tabata Shule na Kawe, Dar es Salaam, ambapo kwenye ukaguzi huo amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji Kata na Polisi Kata kuendelea kuhamasisha vikundi vya ulinzi shirikishi, ili kuhakikisha matukio ya uhalifu yanapungua kwenye maeneo yao.

Pia IGP Sirro amewataka madereva hasa wa pikipiki maarufu bodaboda, kufuata masharti ya leseni zao na kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu wa kutumia nguvu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live