Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa matatani kwa kuingiza simu gerezani, kujirekodi waki-rap kisha kuposti TikTok

Wafungwa Mdkd.jpeg Wafungwa

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafungwa katika gereza la Salford nchini Uingereza wanaripotiwa kuingiza simu gerezani kinyemela kabla ya ku’shoot video yao wakiimba wimbo wa rap na kisha kuipakia kwenye mtandao wa YouTube na Tiktok.

Inaarifiwa kuwa walinzi wa gereza hilo hawakuwa wanajua kilichokuwa kikiendelea muda wote huu ambapo njama ilipangwa ya kuingiza simu na na kufanya video yao wakijivinjari kwenye video.

Video hiyo ya muziki, ambayo imekuwa na maelfu ya watu waliotazamwa, inawaonyesha wafungwa wa Forest Bank wakitoa maneno ya wimbo wao wa kufoka wakiwa seli na kwenye mrengo wa magereza.

Klipu hiyo ya dakika mbili, 'iliyorekodiwa na mandem wote', ina rappers wawili wanaoitwa L1 Manny na Mazza L20.

Washiriki wanaweza kuonekana wakiwa wamefunika nyuso zao na kutengeneza ishara za bunduki kwa mikono yao huku wakipiga mashairi.

Watazamaji wanaofika mwisho wa video wanaelekezwa kwenye akaunti kadhaa za Instagram ikiwa ni pamoja na moja ya Manny, mmoja wa marapa hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live