Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa 800 waliotoroka gerezani DRC wasakwa

Magereza Wafungwaa.jpeg Wafungwa 800 waliotoroka gerezani DRC wasakwa

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikosi vya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vinawasaka zaidi ya wafungwa 800 walioachiliwa huru na waasi wenye silaha.

Jeshi na vyanzo vingine vilisema maafisa wawili wa polisi na muasi mmoja waliuawa katika shambulio katika gereza kuu la Kakwangura, katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Takribani 50 kati ya waliotoroka walikamatwa tena. Wapiganaji wa ADF, kundi linalohusishwa na kundi la Islamic State, wanalaumiwa kwa uvunjaji wa gereza, ambao uliripotiwa kumwachilia huru kiongozi wa waasi.

Ripoti moja ilisema watu wa eneo hilo waliwapiga kwa mawe hadi kuwaua wapiganaji watatu wa ADF. Kundi hilo limeua maelfu ya watu mashariki mwa DR Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live