Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafugaji wavamia nyumba za askari, waiba vyakula, waharibu mali

FF119B29 9325 4518 83B7 153B919D6376.jpeg Wafugaji Morogoro wavamia nyumba za askari, waiba vyakula, waharibu mali

Tue, 20 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Kundi la wafugaji jamii ya Wamang’ati wakiwa na silaha za jadi wanadaiwa kuvamia nyumba za makazi ya maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika shamba la miti la serikali la Pagale lililopo Mvomero mkoani Morogoro kisha kuharibu na kuiba mali zikiwemo sare za askari wa uhifadhi na kusababisha hasara zaidi ya Sh30 milioni.

Akizungumza jana Desemba leo 19, 2022 mkoani hapa, Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti la Mtibwa, Abdallah Mchomvu amesema tukio hilo limetokea usiku wa Desemba 14, 2022 kwa wafugaji hao kuvamia makazi ya nyumba ya askari na kufanya uharibifu kwa kuiba mahindi gunia 30 baada ya kuvunja milango na madirisha.

Mchomvu amesema tukio hilo wanahisi limetekelezwa na wananchi wanaoishi karibu na msitu huo ambao ni waathirika walioondolewa kisheria katika msitu wa Pagale na wafugaji wanaopingana na sheria za uhifadhi kwa kundi hilo kuiba vyakula yakiwemo magunia 30 ya mahindi, viroba 10 vya ngano vya kilo 25 na mtambo mmoja wa kufua umeme wa jua (sola).

“Kundi hili la wafugaji na wananchi wanaoishi karibu na msitu wa Pagale ni waathirika waliondolewa kisheria katika maeneo ya misitu ya TFS lakini na mashamba ya miti, ndio wametekeleza uhalifu huu kwa sababu ya chuki ya kuondolewa ama kuzuiliwa wasihalibu miti iliyopandwa na wameweza kufanya uharibifu kwa kuvunja madirisha 14, milango minane, kuiba vyakula,” amesema hifadhi huyo mkuu.

Ofisa mhifadhi shamba la miti la Pagale, Abdalla Msenga amesema siku ya tukio saa 9 alasiri wao walipata taarifa ya wafugaji kuingiza mifugo katika shamba la miti na askari walikwenda eneo la tukio na wengine kulinda kambi.

“Wenzetu walichelewa kurudi na ilipofika saa 4 usiku tulisikia kelele za wafugaji wakiongea kilugha lakini tuliona mwanga wa tochi na tuliona amani sio salama na tuliamua askari sita kupanda juu ya dali ya nyumba kujificha na walipofika eneo la nyumba walivunja milango, madirisha na kuiba mali mbalimbali,” amesema Msenga.

Msenga amesema walitoa taarifa za siri kwa wenzao na kufika eneo hilo na askari polisi na kundi hilo liliondoka na wao kupata nafasi ya kunusurika na maisha yao.

Ofisa msaidizi misitu wa TFS, Ibrahim Mussa amesema tukio hilo sio la kwanza kutokea kwa askari kuvamiwa na wafugaji ama wananchi waliondolewa kisheria katika shamba la miti la Pagale.

“Kumekuwa na matukio mengi ya wafugaji kuingiza mifugo ndani ya hifadhi ya msitu na Oktoba 29, 2022 lilitokea tukio la sisi kuvamiwa na wakati tunaondoa mifugo wafugaji walikuja juu kwa kutushambulia na baadhi yetu tuliumia lakini tulifanikiwa kuwakamata baadhi yao,” amesema Mussa.

Chanzo: Mwananchi