Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafugaji wajeruhi viongozi watatu Kilosa

Jidy Majid Mwanga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mkata Kati kijiji cha Mkata na viongozi wawili wa dini wamejeruhiwa baada ya kuwashambulia kwa fimbo na kundi la vijana wanaodaiwa kuwa jamii ya wafugaji.

 Kindi hilo linadaiwa kuwashambulia viongozi hao ambao wanahamasisha shughuli ya uwekaji anwani za makazi na postikadi huku vijana hao wakipinga shughuli hiyo.

Mchungaji wa kanisa la Pentekostu Church kijiji cha Mkata, Adam Mwangi amesema tukio la kushambuliwa lilitokea jana usiku wakati akienda dukani kununua mahitaji.

Amesema kabla ya kuondoka alipata taarifa za mtu mmoja kujeruhiwa na kundi la vijana hao baada ya kushambuliwa na kutakiwa kuondoka eneo hilo haraka kuwa ni miongoni mwa viongozi wanaolengwa na kundi hilo kushambuliwa.

“Nilivyoelezwa niliondoka kwa kuchukua tahadhari zote kuanza kukimbia lakini lile kundi la vijana wa kimasai halikuwa mbali na waliniona na kunitambua na kunifukuza na kama mita 100 walinifikia na kuanza kunishambulia kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wangu.” amesema Mchungaji Mwangi.

Amesema wakati vijana hao wanamshambulia, mmoja alikuwa anamuuliza maswali kuwa yeye ni mvamizi kijijini hapo na kama yupo tayari kuhama na yeye ni nani na anafanya nini.

Advertisement “Nilijibu kama walivyotaka kwa kuwa eleza kuwa mimi ni mchungaji kanisa la Pentekosti Church Mkata, nipo tayari kuhama na shughuli ninayofanya ni mtumishi wa Mungu ndio sababu ya kupona au kunusurika na kifo maana kundi lilikuwa kubwa na sijui ile busara ya mmoja wa vijana wa kimasai ilitoka wapi.amesema Mchungaji Mwangi.

Amesema yeye na watumishi wenzake wa makanisa la Anglinana na Katoliki wamekuwa wakihamasisha wananchi kujitokeza kutoa ushirikiano katika uwekaji wa anwani za makazi na postikadi.

Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kimamba, Kasius Kumenya ambaye naye alishambuliwa amesema vijana hao wamefanya vurugu wakipinga uwekaji anwani za makazi huku wakiharibu baadhi ya vibao vya majina ya mitaa.

“Zoezi hili la anwani za makazi na postikadi wafugaji hawataki na sisi kama viongozi wa dini na Mwenyekiti wa Kitongoji ndio tuliolengwa kwani kama viongozi wa dini tulikuwa tunasapoti Serikali kutoa elimu ya wananchi kushiriki zoezi hili na sense.”amesema

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaji Majid Mwanga amesema kwa wanalifuatilia tukio hilo.

Kamati ya Ulinzi na Usalama imefika kijiji cha Mkata kwa lengo la kukutana na viongozi ili kujua chanzo cha vurugu hizo kwa viongozi hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live