Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi Chadema Waongeza Presha Kesi ya Mbowe Kisutu

CHADEMA 222 Wafuasi wa CHADEMA

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Jeshi la Polisi kusisitiza wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wasifike katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekuwa tofauti kabisa na maelekezo hayo waliyo yatoa.

Wafuasi hao wameonekana Mahakamani hapo kwa wingi wakiwa na mabango yanasosisitiza kuwa Mwenyekiti wao Freeman Aikael Mbowe sio Gaidi kama inavyodaiwa na jeshi la Polisi.

Hata hivyo pia viongozi wa ndani ya chama hicho wakiongozwa na katibu Mkuu wa Chama John Mnyika, wameonekana kwenye viunga vya Mahakama hiyo tayari kwa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomakabili kiongozi wao.

Mbowe alikamatwa tarehe 21 Julai Mwaka huu akiwa Jijini Mwanza kwenye kongamano la Baraza la vijana Chadema BAVICHA , lililokuwa likishinikiza upatikanaji wa Katiba Mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live