Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi 31 Chadema kusomewa maelezo Januari, 2019

Fri, 14 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Januari 21, 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itawasomea maelezo ya awali watu 31 wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amedai leo Alhamisi Desemba 13, 2018  mbele ya Hakimu mwandamizi Augustine Rwizile kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Februari 16, 2018 Mkwajuni wilayani Kinondoni watu hao wanadaiwa kufanya mkusanyiko usio wa halali na kinyume cha sheria

Washtakiwa katika kesi hiyo ya jinai namba 51/2018 ni Thabita Mkude, Haji Lukwambe, Emmanuel Kimoi, Mohammed Juma, Hussein Mrombo, Abdallah Hamis, Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein Nguli, Edna Kimoro.

Wengine ni Jonathan Lema, Salha Ngondo, Ramadhan Mombo, Godwin Mwakasungura, Hassan Kibweda, Omary Hamad, Fatima Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa, Dickson Kerefu, Raphael Mwaipopo, Athuman Mkawa, Mussa Kusigila.

Wakili wa utetezi Gaston Shundo alidai kuwa kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama zilitaka upande wa Mashtaka kukamilisha upelelezi kwa kuwa wameshakamililisha hakuna pingamizi.

Baada ya kuelezwa hayo Hakimu Rwizile amewataka wadhamini wa washtakiwa hao kuhakikisha wanafika kwenye shauri hilo bila kukosa katika tarehe itakayopangwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 21, 2019. Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.



Chanzo: mwananchi.co.tz