Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafikishwa kortini kwa rushwa na kumtorosha mtuhumiwa

8fe2d5075a169ddd4fa15dffbb29cf20 Wafikishwa kortini kwa rushwa na kumtorosha mtuhumiwa

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika Mkoa wa Rukwa, imewafi kisha mahakamani Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kipanga, Jacob Masolwa na Ofi sa Mtendaji wa Kijiji cha Kipanga, Ronald Katito kwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh 360,000 na kumtorosha mtuhumiwa.

Wameshitakiwa kwa kuomba na kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa wazazi wa mshitakiwa Justine Kandoro anayedaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 16.

Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Rukwa, Yustina Chagaka, alibainisha hayo mjini hapa wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu.

Alisema washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo hivi karibu katika Kijiji cha Kipanga kilichopo katika Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

“Baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kuzuiliwa katika mahabusu ya Kijiji cha Kipanga aliachiwa baada ya washitakiwa hao kuomba na kupokea rushwa ya Sh 360,000 kutoka kwa wazazi wa mtuhumiwa... Mtuhumiwa Justine ametoroka na kwenda kujificha kusikojulikana, maofisa wa taasisi wanaendelea kumsaka,” alieleza.

Alisema Mahakama ya Wilaya ya Kalambo imewaachia kwa dhamana washtakiwa hao baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Chagaka alisema katika kipindi hicho Takukuru imeendelea na uendeshaji wa mashtaka mbalimbali katika mahakama za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo na tayari mashtaka 12 ya uchunguzi yamekamilika na mengine yamefunguliwa kesi mahakamani.

Aidha, kesi mpya nne zimefunguliwa katika kipindi cha Januari hadi Machi, hivyo kufanya idadi ya kesi tisa zinazoendelea kusikilizwa mahakamani huku kesi moja ikiwa tayari imetolewa hukumu baada ya kumtia hatiani mtuhumiwa

Chanzo: www.habarileo.co.tz