Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi Fastjet waitaka Serikali kuzing’ang’ania ndege mbili

45201 Fastpic Wafanyakazi Fastjet waitaka Serikali kuzing’ang’ania ndege mbili

Thu, 7 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyakazi zaidi ya 120 wa Kampuni ya Ndege ya Fasjet Tanzania wameiomba Serikali kuendelea kuzishikilia ndege mbili za kampuni hiyo mpaka pale madai yao ikiwamo mishahara itakapolipwa.

Wafanyakazi hao wamesema wanaidai kampuni hiyo Sh2.75 bilioni za mishahara na madai mengine kama michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Machi 6, 2019 wafanyakazi hao wamesema kama ndege hizo zikiachwa ziondoke itakuwa vigumu kupata haki zao.

"Ndege hizi moja ipo hapa Dar es Salaam na moja Nairobi na ikiwa zitazuiwa tutalipwa madai yetu, kwa hiyo tunaiomba Serikali isizifutie huo usajili au kuruhusiwa kuondoka nchini kabla ya kulipwa madai yetu," amesema mmoja wa wafanyakazi hao Mohammed Ngamanya.

Ngamanya amesema mwajiri wao ni sehemu ya Fastjet PLS kutoka nchini Afrika Kusini na kwamba, changamoto za kiuongozi ndizo zilizoifikisha kampuni hiyo ilipo.

Amesema Serikali imetoa mwongozo kuwa ili ifungwe lazima taratibu zote za kisheria zifuatwe ikiwamo kulipwa madai yao, lakini haikuwa hivyo kwa sababu ilifungwa ghafla.

Ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA) unaoratibu safari za anga za mashirika ya ndege nchini wasitambue au kukubali ubadilishanaji wa umiliki wa kampuni hiyo hapa nchini.

"Tunapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa kinachoendelea Fastjet sio sababu za kisiasa kama wengi wanavyodhani, bali ni matatizo ya kiutendaji ya mwajiri wetu ambaye ni Fastjet PLC," amesema Ngamanya.

Kwa upande wake, Ofisa Mwendeshaji Mkuu upande wa uwanja wa ndege, Alex Njoge amesema wanamtambua Lawrence Masha kama mfanyakazi mwenzao na mjumbe wa bodi.

Ofisa Rasilimali Watu wa Fastjet Tanzania, Emmanuel Muhindi amesema madai ya wafanyakazi hao ni sahihi na kwamba, hawajaweza kuwalipa mshahara wa mwezi wa pili japokuwa walimudu kuwalipa nusu ya mishahara baadhi ya wafanyakazi kwa mwezi Januari.

Wafanyakazi waiomba TAA ishikilie ndege za Fastjet

 



Chanzo: mwananchi.co.tz