Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara waikosesha mapato Z’bar kwa magendo

8847 Zanzibar+pic TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Joseph Abdalla Meza amesema licha ya mafanikio katika ukusanyaji wa kodi bado kuna mapato yanakosekana kutokana na magendo yanayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.

Meza alisema hayo juzi baada ya mkutano wa 44 wa makamishna wa mamlaka za mapato kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Gulioni mjini Unguja.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara wasiopenda maendeleo huanzisha bandari zisizo rasmi (bubu) kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.

Kamishna wa Mapato ya Ndani nchini Rwanda, Kayigi Aimable alisema mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato yanatokana na elimu ya mlipakodi inayotolewa.

Alisema ni vyema nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza elimu kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kulipa kodi.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema wamedhamiria kuandaa sheria ya pamoja kuwabaini wanaokwamisha ukusanyaji mapato ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Chanzo: mwananchi.co.tz