Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara 12 wadakwa wakidaiwa kubadilisha fedha bila kuwa na kibali

70435 Bandia+pic

Thu, 8 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Wafanyabiashara 12 wa mkoani Tanga  wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila ya kuwa na leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akizungumza jana Jumatano Agosti 7, 2019 kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga, Leons Rwegasira amesema wafanyabiashara hao wamekamatwa baada ya polisi kufanya msako kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Dola.

Amesema katika msako huo uliofanyika kwenye maduka na sehemu mbalimbali, wafanyabiashara hao walinaswa na dola za Marekani 65,961 na Sh63.3 milioni.

Pia, zimekamatwa Sh236,549 za Kenya; Euro 270, Paundi ya Uingereza 400, Randi 1,020 ya Afrika Kusini, Rial  521 ya Oman, Sh2,000 ya Uganda na Rupia 1,349.

Kaimu Kamanda huyo amesema katika operesheni hiyo wamekamata  fedha na madini bandia.

Amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa mahojiano, uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz