Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waethiopia wanaswa wakitimkia kwa Madiba...

Mbaroni Waethiopia.png Waethiopia wanaswa wakitimkia kwa Madiba...

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari ya raia wanne wa Ethiopia waliopenya nchini kwa lengo la kuelekea Afrika Kusini bila kuwa na vibali imeishia mkoani Iringa baada ya jeshi la Polisi kuwanasa katika kizuizi cha Polisi Changarawe wilayani Mufindi.

Akizungumza na wanahabari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema waethiopia hao walikamatwa Mei 22, mwaka huu wakiwa kwenye gari mbili tofauti (IT) zilizokuwa zinapelekwa Zambia.

"Waethiopia hao walikuwa wakielekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kwa kutumia gari hizo ambazo ni IT 3802 aina ya Vits na IT 7485 aina ya mazda," amesema.

Amesema wakati Vits ilikuwa ikiendeshwa na Musa Omari (32) mkazi wa Tabata Dar es Salaam, Mazda ilikuwa ikiendeshwa na Musa Mashala mkazi wa Airport Dar es Salaam.

Wakati majina ya waethiopia wawili hayajajulikana kwasababu ya changamoto ya lugha, Kamanda Bukumbi aliwataja wawili wengine kuwa ni Tesfahun Petros (22) na Degefe Sugumo (20).

"Watuhumiwa hao kwa pamoja wanashikiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani pamoja na magari hayo yatapelekwa kama vielelezo," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live