Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waethiopia 9 wakamatwa Handeni

Waethipoia Waamaiji Hyandeni Waethiopia 9 wakamatwa Handeni

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Jeshi la Uhamiaji wilayani Handeni mkoani Tanga limewakamata raia tisa wa Ethiopia pamoja na Mtanzania mmoja wakiwa wamefichwa kwenye shamba la michungwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumapili Septemba 25 2022, Kaimu Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Handeni, Mkumbo Gideon amesema raia hao walikuwa wamefichwa katika Kijiji cha Ngojolo, Kata ya Kwamgwe wakisubiria usafiri kwa ajili ya kuendelea na safari.

Amesema pia wamemkamata Mtanzania, Hassani Ramadhani anayetuhumiwa kuratibu usafiri wa wahamiaji hao.

"Tumefanikiwa kukamata raia tisa wa Ethiopia walioingia kinyume cha sheria na Mtanzania mmoja Hassani Ramadhani mkazi wa Hale, ambae tuna mtuhumu kwa kutenda kosa la kusafirisha wahamiaji haramu, wote tunawafikisha mahakamani," amesema Mkumbo.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema wiki iliyopita pia walikamatwa raia watatu wa Ethiopia, hivyo kwa idadi hiyo watakuwa wamefikia 12.

Amesema kata ya Kwamgwe imeonekana ni kituo cha kupitisha wahamiaji haramu wakitokea Michungwani na Hale, hivyo kuwapongeza wananchi kwa kutoa taarifa juu ya watu hao.

Advertisement "Ni aibu sana kumuona Mtanzania unahujumu usalama wa nchi yako kwa kushirikiana na watu hawa.

“Tulishakamata mwanamke mmoja ambaye pia alipakia wahamiaji haramu kwenye gari lenye vioo vyeusi," amesema Mchembe.

Kadhalika mkuu huyo wa wilaya ameviomba vya habari kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za masuala ya upitishwaji wahamiaji haramu na serikali itatoa ushirikiano kwao.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz