Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadakwa na noti bandia za Sh2milioni

30315 Helabandiapic TanzaniaWeb

Thu, 6 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)  limewakamata watu watano wanaodaiwa kuwa majambazi kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia za Sh2.83 milioni.

Watu hao pia wamekamatwa na vifaa mbalimbali vya kutengeneza noti hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano  Desemba 5, 2018 Kamanda wa polisi mkoani humo,  Jonathan Shanna amesema watu hao wamekamatwa  katika operesheni maalumu iliyofanyika Desemba 3 na 4, 2018  katika mtaa wa Kiloleli B,  kata ya Nyasaka wilayani Ilemela.

“Operesheni hiyo iliyochukua saa 48 imefanyika baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa kuna watu wanatengeneza noti bandia,” amesema Shanna.

Amesema kati ya watu hao wawili wamekamatwa wakiwa wilayani Mugumu Serengeti ambao ni Swedi Mrete (40) mfanyabiashara na Cosmas Bereke (40), fundi chuma wote wakazi wa Mwanza.

Wengine ni Baraka Dominiko (26), Khadija Elias (20) na Batisti Katumbi (40).

Noti zilizokamatwa ni za 10,000; 5,000; 2,000 na noti 18 za Dola mia moja ya Marekani, zote zikiwa na thamani ya Sh2.83milioni.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na Printer, paper cutter moja, pasi tatu za umeme, cartilage nane, Ink Refuels chupa nane, sirinji nne na Rim paper.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz