Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadakwa kwa wizi TANESCO

Umeme REA CCM Wadakwa kwa wizi TANESCO

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuingilia miundombinu ya Tanesco katika soko la Kariakoo na kuisababishia hasara ya zaidi ya Sh 316 milioni

Washtakiwa hao ni Erick Rushenzirane (20), Emanuel Daroshi (30) na Baruani Baruani (29) wote ni wakazi wa Temeke

Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava alisoma hati ya mashtaka alidai Januari 14,2022 maeneo ya soko la Kariakoo wote kwa pamoja waliiba vifaa vya umeme katika miundombinu ya Tanesco na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 316,980,333.48

Upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine Kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mkazi Mkuu,Ramadhani Rugemalira alisema washtakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote Kwa kuwa shitaka wanalokabiliwa nalo ni la uhujumu uchumi.

"Washtakiwa mnaweza kupata dhamana ila mahakama hii haina uwezo yenye mamlaka ni mahakama kuu ya Tanzania hivyo naahirisha kesi hii hadi Machi 2, 2022 na washtakiwa wote mtaaenda mahabusu,"alisema Rugemalira

Chanzo: www.tanzaniaweb.live