Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji wawili wa madini wauawa Mbeya

E5a8dbb0ef259de8295159d2aa05bd0f.jpeg Wachimbaji wawili wa madini wauawa Mbeya

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachimbaji wawili wa madini wameuawa katika matukio mawili tofauti yaliyotokea mkoani Mbeya, likiwamo la mmoja kupigwa na sururu kichwani wakati yeye na wachimbaji wenzake wakigombania chakula.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ilieleza kuwa, mchimbaji aliyeuawa kwa kupigwa sururu ni Mhoja Mihambo (30) mkazi wa Kitongoji cha Ujerumani, Kata ya Mkola, wilayani Chunya.

Alisema kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi linamshikilia mchimbaji Masele Lige (30) mkazi wa Kitongoji cha Ujerumani kwa tuhuma za mauaji hayo, huku likiendelea kumsaka mchimbaji mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Clement aliyekimbia baada ya tukio.

Kamanda Matei alisema

tukio hilo lilitokea Desemba 24, mwaka huu, saa 12:00 asubuhi katika Kitongoji cha Ujerumani kilichopo Kata ya Mkola, Tarafa ya Kiwanja wilayani Chunya.

Alisema chanzo cha tukio ni kugombania chakula kwa madai kwamba marehemu alikua hatoi michango ya chakula mara wauzapo dhahabu.

“Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo kwa kushirikiana na mwenzake. Msako mkali unaendelea kumtafuta mtuhumiwa aliyekimbia na upelelezi wa shauri hili unaendelea,” alisema.

Katika tukio jingine, Kamanda Matei alisema jeshi hilo linamsaka mtu anayefahamika kwa jina moja la Lole mkazi wa Kijiji cha Kiwanja wilayani Chunya kwa tuhuma za mauaji ya Samwel Chisunga (19) mkazi wa wilayani Mbozi mkoani Songwe kwa kumshambulia mwenzake sehemu mbalimbali za mwili kwa

kutumia fimbo. Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu saa 11:00 alfajiri katika Kijiji cha Mlimanjiwa kilichopo Kata ya Mbugani, Tarafa ya Kiwanja wilayani Chunya.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni marehemu kudaiwa kuiba unga udhaniwayo kuwa na dhahabu maarufu kwa jina la Omega mali ya mtuhumiwa na kuongeza kuwa, msako wa kumtafuta mtuhumiwa ambaye alitoroka baada ya kutenda tukio hilo unaendelea.

Wakati huo huo, Kamanda Matei alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa wa mauaji yaliyotokea Agosti 14, mwaka 2019, Msumbuko Patson (31) mkazi wa Kijiji cha Matundasi wilayani Chunya aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi hilo.

Alisema Patson ambaye alikamatwa Desemba 25, mwaka huu saa 2:00 usiku katika msako uliofanyika katika Kata ya Matundasi anashikiliwa na polisi kwa tuhuma

za mauaji ya Ndugusu yaliyotokea mwaka 2019 na kisha kukimbia.

Alisema mtuhumiwa baada ya mahojiano na jeshi hilo alikiri kosa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Matei alisema polisi pia inamsaka Sombwile Mwakasambwe mkazi wa Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani hapa kwa tuhuma za kumjeruhi mkazi mwenzie Paulina Mwaikupa (41) kwa kumshambulia na kitu chenye ncha kali.

Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu saa 5:00 usiku katika Kijiji na Kata ya Ikolo, wilayani Kyela na chanzo ni tamaa za kingono kwani inaelezwa wakati wa tukio muathirika alikuwa amelala ndani ya nyumba yake ghafla mtuhumiwa aliingia kwa nia ya kufanya shambulio la aibu lakini alipomwona alipiga kelele za kuomba msaada ndipo kwa hasira alitoa kisu na kumjeruhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live