Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezea kichapo kizito kwa kutaka kuiba dukani Mwenge

Vijana Mwenge Wachezea kichapo kizito kwa kutaka kuiba dukani Mwenge

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wawili ambao majina yao hayajafahamika wamepigwa na Wananchi wenye hasira kali baada ya kuvamia duka la michezo ya kubahatisha (betting) na kutaka kupora fedha katika eneo la Mwenge (Kituo cha Daladala cha ITV).

Kwa mujibu wa Shuhuda, Vijana hao walivamia duka hilo wakiwa na mawe na wamemjeruhi Dada anayetoa huduma kwenye duka hilo kwa kumpiga jiwe usoni na amepelekwa Hospitali.

Shuhuda mwingine anadai Vijana hao walikuwa watatu na walifika eneo la tukio kwa kutumia pikipiki ambapo mmoja alifanikiwa kutoroka baada ya kuona hatari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live