Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa Chadema na wenzao saba wapelekwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi

44376 MOROPIC Wabunge wa Chadema na wenzao saba wapelekwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi

Sun, 3 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro.  Wabunge wawili wa Chadema Suzan Kiwanga, Peter Lijualikali na wenzao saba wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.

Wabunge hao na wenzao wameletwa mahakamani hapo leo Ijumaa, Machi 1, 2019 kwa ajili ya kusikiliza maamuzi ya mahakama kuhusu dhamana yao ambayo ilipingwa na upande wa mashtaka kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya kukwamisha kupatikana kwa washtakiwa wengine wanne.

Wakati washtakiwa wakifikishwa mahakamani hapo wafuasi wa Chadema wakionekana kukaa mbali kuhofia askari waliowasindikiza wabunge hao kutoka mahabusu.

Wabunge hao na wenzao saba wanashitakiwa kwa makosa nane likiwemo la kuharibu mali na kuchoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji cha Sofi wilayani Malinyi.

VIDEO: Wabunge Chadema wasota rumande

 



Chanzo: mwananchi.co.tz