Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Chadema kortini, tuhuma hazijajulikana

43671 Pic+wabunge Wabunge Chadema kortini, tuhuma hazijajulikana

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Kilombero) na Susan Kiwanga wa Mlimba na wenzao saba wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kukamatwa na polisi.

Wabunge hao walikamatwa Jumatano iliyopita ya Februari 20, 2019 wakiwa Kijiji cha Sofi wilaya ya Malinyi na kukaa rumande hadi leo Jumatatu Februari 25, 2019.

Akizungumza na Mwananchi, Kaimu Katibu wa Vijana Chadema mkoa wa Morogoro, Jackson Malisa amesema wabunge Lijualikali na Kiwanga wamekutwa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi kituo kikuu cha Morogoro.

"Waliokamatwa kijiji cha Sofi ni pamoja na aliyekuwa mgombea kiti cha udiwani kata ya Sofi mwaka juzi katika uchaguzi mdogo, Liko Likomo pamoja na wanachama sita, wabunge wawili na kufanya idadi yao kuwa tisa." alisema Malisa.

Malisa amesema bado haijafahamika wabunge hao na wenzao wana tuhuma gani na wanaendelea kufuatilia.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri mahakamani hapo



Chanzo: mwananchi.co.tz