Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandishi wa Habari 1,700 wauawa duniani

7C484193 D0F5 4A1C AADE 9C46812D7EE6.jpeg Waandishi wa Habari 1,700 wauawa duniani

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: dar24

Katibu Mkuu wa Shirika la Waandishi Habari wasio na Mipaka (RSF), Christophe Deloire amesema takribani waandishi habari 1,700 wameuawa duniani kote katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Deloire, ameyasema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari na kuongeza kuwa, waliouawa ni wale waliojitolea maisha yao kwa ajili ya kukusanya taarifa, kufanya utafiti wa kupata ukweli na shauku yao ya uandishi habari huku akizutaja Iraq na Syria kama moja ya nchi ambazo ni hatari kufanya kazi za uandishi. 

Amesema, jumla ya waandishi habari 578 wameuawa kwenye nchi hizo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na kwamba I dadi hiyo inafuatiwa na waandishi habari 125 waliouawa Mexico, 107 Ufilipino, 93 Pakistan, 81 Afghanistan na 78 Somalia.

Aidha, kwa upande wa bara la Ulaya Uturuki imeshika nafasi ya tatu kama nchi hatari zaidi kufanya kazi za uandishi wa Habari, ikifuatiwa na Ufaransa kutokana na mauaji ya wafanyakazi wa jarida la vibonzo la Charlie Hebdo jijini Paris, mwaka 2015.

Chanzo: dar24