Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waachiwa kesi ya rushwa milioni 30/-

B06261396a42642767a4ae6198071318.png Waachiwa kesi ya rushwa milioni 30/-

Mon, 3 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Wilaya ya Arusha imemwachia huru mfanyabiashara wa madini ya tanzanite, Lucas Mdeme (46) na mwenzake, Nelson Lyimo (58).

Mdeme na Lyimo walikuwa wakikabiliwa na mashitaka sita likiwamo la uhujumu uchumi.

Mahakama hiyo imewaachia huru baada ya upande wa mashitaka kueleza hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Katika kesi hiyo, Mdeme na Lyimo waliokuwa ni miongoni mwa washitakiwa wanane wakiwamo polisi watatu.

Mashitaka katika kesi hiyo yanahusu uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia rushwa ya fedha ya awali Sh milioni 10 kati ya Sh milioni 30 walizohitaji kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Arusha.

Mfanyabiashara huyo, Sammy Mollel pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wauzaji Madini Wakubwa ndani ya nchi na nje (Tamida).

Waendesha mashitaka wa serikali, Adelaide Kassalay na Agnes Hyera walimweleza Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Rose Ngoka kuwa, upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo na na kuiomba iwaachie huru.

''Mheshimiwa Hakimu upande wa Jamhuri hatuna nia ya kuendelea na mshitakiwa namba sita na saba katika shauri hilo, hivyo tunaiomba Mahakama iwaachie huru bila masharti yoyote,'' alisema Kassalay.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ngoka aliamuru kuachiwa huru, Mdeme na Lyimo na akaahirisha kesi hiyo hadi kesho.

Askari waliopandishwa kizimbani baada ya kufukuzwa kazi ni mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi aliyekuwa kitengo cha Intelijensia mkoa wa kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, H.125 PC Gasper Paul kitengo cha intelijensia makao makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa askari wa kawaida mkoani Dodoma.

Washitakiwa wengine ni Joseph Chacha (43) mkazi wa Ilboru, Leonila Joseph (46) mkazi wa Ilboru na Omary Alphonce (43) mkazi wa Olasiva jijini Arusha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz