Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wa 5 kortini kwa tuhuma kutakatisha mil.365/-

4654a0ff98a3bfefd99cff420225786b Wa 5 kortini kwa tuhuma kutakatisha mil.365/-

Tue, 8 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU watano wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka 14 ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kughushi na kutakatisha Sh milioni 365.

Washtakiwa hao wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni Reginald Masawe, Garston Danda, Cladius Kabwogi, Irene Marwa na Noel Kitundu.

Walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu. Akiwasomea mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu Martenus Marandu alidai katika shtaka la kwanza la kuongoza genge la uhalifu washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Desemba 2019 na Novemba 2020 jijni Dar es Salaam, kwa kukusudia waliongoza genge la uhalifu, kufoji na kutakatisha.

Katika shtaka la pili linalomhusu mshtakiwa wa kwanza na wa pili, inadaiwa walighushi fomu ya maombi ya Benki ya ABC Tawi la Tegeta na kutoa nyaraka feki kwa lengo la kutaka kupata taarifa za mteja mwenye akaunti katika tawi hilo.

Katika shtaka la 3 mpaka 7 inadaiwa mshtakiwa Reginald Masawe alighushi nyaraka mbalimbali ikiwemo leseni ya biashara, hati ya Namba ya Mlipa Kodi (TIN), fomu ya kufungua akaunti katika Tawi la Benki ya NMB Msasani, akijifanya ni mfanyakazi wa Tanesco mwenye jina la Riziki Kayenga, kosa analodaiwa kulifanya pia katika shtaka la tano na la sita.

Katika shtaka la saba na la nane, Masawe anadaiwa kughushi fomu ya mkopo katika Tawi la NMB Mlimani City, akijifanya yeye ni Riziki Kayenga na kughushi ‘slary slip’ yake.

Katika shtaka la tisa alitoa nyaraka za uongo kwa maofisa wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City kwa ulaghai akiijifanya ni Riziki Kayenga, mfanyakazi wa Tanesco, akionesha kuwa ni nyaraka halali huku akijua si kweli.

Wakili Marandu aliendelea kudai kuwa katika shtaka la kumi, linalowakabili washtakiiwa wote inadaiwa manamo Desemba 28 2019 washtakiwa wote walijipatia mkopo wa Sh milioni 65 kutoka Benki ya NMB Tawi la Mlimani City pale ambapo mshtakiwa namba moja, alijifanya mfanyakazi wa Tanesco huku akijua si kweli.

Alidai katika shtaka la kumi na moja mnamo Desemba 28, 2019 washtakiwa wote walijipatia mkopo wa Sh milioni 50 kutoka Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, ambapo mshtakiwa Masawe alijifanya ni mfanyakazi wa Tanesco huku akijua si kweli.

Katika shtaka la kumi na mbili, inadaiwa washtakiwa wote kwa pamoja walijipatia mkopo wa Sh 34, 200,000 kutoka Bnki ya CRDB Tawi la Msasani kupitia akaunti ya mshtakiwa namba nne, Irene Marwa ambaye alijifanya ni Martha James, kosa wanalodaiwa kulifanya Septemba 8, 2020.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la kumi na tatu, washtakiwa hao mnamo Oktoba 2, 2020 walijipatia mkopo wa Sh milioni 50 kutoka Benki ya CRDB Tawi la Msasanj kupitia akaunti ya mshtakiwa namba tano, Noel Kitundu ambaye alijifanya ni Michael Mwang'onda.

Katika shtaka la mwisho la kutakatisha fedha, inadaiwa washtajiwa hao kwa pamoja kwa nia ovu kati ya Desemba 2019 na Novemba 2020 katika jiji la Dar es Saalaam, walijipatia Sh milioni 365 mali ya Tanesco, wakijua ni masalia ya uhalifu

Chanzo: habarileo.co.tz