Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA MAUWAJI

Image 292.png?fit=575%2C436 WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA MAUWAJI

Fri, 14 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Watu wawili wahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatiani ya kuhusika na mauaji ya mtu mmoja katika eneo la Kitendaguro katika Manispaa ya Bukoba yaliyotokea Machi 9, 2015, huku mtuhumiwa mmoja akiachiwa huru.

Hukumu hiyo ya kesi namba 34 ya mwaka 2020 imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo Sam Rumanyika baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamanihapo dhidi ya watuhumiwa hao.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo Mkurugenzi wa usimamizi wa kesi na uratibu wa upelelezi, kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Hashimu Ngole amesema Serikali imeridhishwa na maamuzi ya Mahakama ambayo yanarejesha imani ya wananchi waliokuwa wakiishi kwa wasiwasi kwa kuhofia kukatwa makoromeo.

Mwaka 2015 yaliibuka mauaji ya kukata watu makoromeo na kuzua hofu kwa wakazi kwa baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Kagera.

Story na Na Lydia Lugakila: Kagera

Chanzo: zanzibar24.co.tz