Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WANNE KIZUIZINI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Security Fraud MED Istock1 WANNE KIZUIZINI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Wed, 14 Oct 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini unguja kwa kosa la kujihusisha na Ubakaji wa Kikundi na kumbaka Mwanamke jina lake linahifadhiwa mwenye umri wa miaka 24 Mkaazi wa Tangi la Maji Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea baina ya tarehe 7 na 8 majira ya saa 4:00 usiku na 7:00 Usiku huko Tangi la Maji Bwejuu .

Amewataja wa mtuhumiwa hao kuwa ni Hafidh Haji maarufu Bakharesa mwenye umri wa miaka 20 , Takrimu Issa Abdalla mwenye umri wa miaka 20 , Fahmi Suleiman Mbaraka maarufu Keita mwenye umri wa miaka 22 pamoja na Hassan Abdalla Abdalla mwenye umri wa miaka 19 wote kwa pamoja ni wakazi wa Bwejuu.

Sambamba na hayo Sheha wa Shehia ya Bwejuu Dongwe Ali Haji Mkadamu amekiri kupokea taarifa hiyo na kuwataka wazazi na walezi wanapaswa kuwa karibu na watoto ili kuweza kujua matendo na kuepusha na matendo ya kianasa .

Story na Rauhiya Mussa Shaaban.

Chanzo: zanzibar24.co.tz