Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WALIMU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUUA MWANAFUNZI

0492df98cd55cc4aff3bb0479c24a427 WALIMU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUUA MWANAFUNZI

Fri, 6 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WALIMU wawili wa shule ya msingi na awali ya Holly Cross ya Mtoni Kijichi jijini Dar er Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shitaka la mauaji ya Cuthbert Chacha anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa shule hiyo.

Washtakiwa hao Leahdorice Agunda na Martha Lizer wamefikishwa mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luboroga na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 14, 2020 katika shule ya Holly Cross iliyopo Mtoni Kijichi, Wilaya ya Temeke jijini Dar ea Salaam.

Simon alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na aliomba tarehe nyingine ya kutajwa shauri hilo. Hakimu Luboroga aliahirisha kesi hiyi hadi Novemba 19, 2020.

Chanzo: habarileo.co.tz