Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyombo vya upelelzi vyapewa jukumu lingine zito

Upeleezi Vyombo vya upelelzi vyapewa jukumu lingine zito

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Utumishi wa Mahakama imevishauri vyombo vya upepelezi nchini kukamilisha uchunguzi wa malalamiko kabla ya kufungua mashauri mahakamani.

Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Tume, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Dk Gerald Ndika hiyo jana mjini Morogoro wakati wa mkutano wa Tume hiyo na wadau wa mahakama Mkoa wa Morogoro.

Katika mkutano huo Jaji Dk Ndika ambaye ni alisema Jeshi la Polisi halina budi kuharakisha upelelezi ili kuongeza kasi ya usikilizwaji wa mashauri na kurahisisha upatikanaji wa haki.

“Kila mdau wa Mahakama anapaswa kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi kwa kuwa mfumo wa utoaji haki unategemeana, Mahakama peke yake haitaweza kutoa haki kwa wakati endapo wadau wake watabaki nyuma,”alisema Jaji Dk Ndika.

Aliwataka majaji na mahakimu nchini kuhakikisha kuwa mashauri yanayopokelewa mahakamani ni yale ambayo upelelezi wake umekamilika ukiacha mashauri ya mauaji ambayo upeplelezi wake huchukua muda mrefu.

Jaji Dk Ndika alisema moja ya majukumu ya Tume hiyo ni pamoja na kufanya uboreshaji wa huduma zinazotolewa na Mahakama nchini hivyo alishauri Uongozi wa Mahakama kutoa ruhusa kwa Mahakimu wenye mamlaka ya ziada (Extended Jurisdiction) kutoa uamuzi kwenye mashauri ili kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani.

Pia, Jaji Dk Ndika alitaka upelelezi wa mashauri yanayowahusisha watoto kukamilika haraka ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa haki kwa wananchi.

“Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, ni vema upelelezi wa maabara ukafikishwa mahakamani kwa haraka na ukiwa umekamilika,”alisema.

Kwa upande wake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapher Siyani alitaja baadhi ya mafanikio ya Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano kuwa ni pamoja na kubadilisha mfumo wa uongozi kupitia Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Namba 4 ya mwaka 2011 imeleta ufanisi katika utendaji kazi wa Mhimili huo.

Alisema kupitia utekelezaji wa mpango mkakati wa awali wa miaka mitano na mpango mkakati mpya wa 2021/2025 Mahakama ya Tanzania imefanya uboreshaji mkubwa wa huduma inazozitoa.

Maboresho hayo ni kujenga majengo ya kisasa na kuingia kwenye matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) iliyosaidia kurahisisha utendaji kazi wa Mahakama.

Alisema Mahakama katika kipindi cha miaka mitano imefanikiwa kuimarisha uwajibikaji unaolenga kupata matokeo ambapo zaidi ya asilimia 77 ya wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na Mahakama.

Jaji Kiongozi alisema, matarajio ya Mahakama kutoka kwa wadau wake ni vyombo vya upelelezi kuzingatia sheria, taratibu na miongozi ili upelelezi ufanyike kwa haraka na kusaidia mashauri kumalizika kwa wakati mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live