Kampuni ya Vodacom imeomba Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini kutoa idhini ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kumlipa mbunifu wa huduma ya ‘Tafadhali Nipigie,’ Kenneth Makate asilimia 5 hadi 7.5 ya mapato yaliyotokana na huduma hiyo kwa zaidi ya miaka 18 iliyotumika.
Kampuni ya Vodacom imeomba Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini kutoa idhini ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kumlipa mbunifu wa huduma ya ‘Tafadhali Nipigie,’ Kenneth Makate asilimia 5 hadi 7.5 ya mapato yaliyotokana na huduma hiyo kwa zaidi ya miaka 18 iliyotumika. Vodacom imesema malipo hayo yataleta athari kwa wafanyakazi wake, wanahisa pamoja na huduma.