Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitisho vya Bastola vyawasweka jela wanne

Bastola Mbaroni matumizi mabaya ya silaha

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Dar es salaam wanawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutisha watu kwa bastola wanazozimiliki kihalali

kamanda Muliro amethibitisha kuwakamata watu hao leo august 4,2012 , maeneo toafuti tofauti jijini humo, alitaja majina ya watuhumiwa hao kuwa ni , Isack Robert Wile maarufu kama Wambura (44), mkazi wa Sinza E, Rashid Iddi Mshana (36) mkazi wa mwenge, Mussa Rashid Mshana (39), mkazi wa Mwenge na Ibrahim Shaibu (52) mkazi wa Kinyerezi.

Mtuhumiwa wa kwanza, Bw. Isack, alifanya tukio la kutisha watu akiwa katika moja ya bar ianyopatikan a sinza, huku mtuhumiwa wapili Bw. Rashid, akionekana katika video iliyosambaa mtandaoni akifanya vitisho vya silaha, mtuhumiwa wa tatu Bw.Musaa, yeye anashitakiwa kwa kosala uzembe wa kumuachia silaha mdogo wake ambae ni mtuhumiwa wa wapili, na mtuhumiwa wa mwisho Bw. Ibrahimu yeye alimtishia kumuua kwa silaha jirani yake wakati wakigombania mipaka ya kiwanja .

Mwezi Julai mwaka huu, Polisi walithibitha kutokea kwa mauaji yaliyo sababishwa na matumizi mabaya ya silaha ikiwemo vitisho, yaliyohusianishwa pia na matumizi ya vileo.

Aidha jeshi la polisi linaendelea kuwataka wanachi kutoa taarifa mara moja pindi wanapoona vitendo vya matumizi mabaya ya silaha vikifanyika .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live