Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi, wafuasi wapiga kambi alikolazwa mwanaharakati wa Tanzania Mdude Chadema

56481 Mdudeeepic

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Viongozi na wafuasi wa Chadema wamepiga kambi nje ya wodi  namba sita Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya alikolazwa Mdude Nyagali maarufu Mdude Chadema tangu alipopatikana usiku wa kuamkia leo Alhamisi Mei 9, 2019 akiwa hai lakini hoi.

Nyagali aliyetekwa na watu wasiojulikana Jumamosi iliyopita akiwa ofisini kwake Vwawa-Mbozi, mkoani Songwe amefikishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

Alifikishwa katika hospitali hiyo jana saa 5 usiku baada ya  kuchukuliwa eneo la Inyala, Mbeya vijijiji alikotelekezwa.

Wasamaria wema walimuona akiwa eneo hilo na kumuokota kisha kutoa taarifa kwa viongozi wa Chadema ambao walikwenda kumchukua usiku.

Viongozi walioko hospitalini hapo ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Sadrick Malila, Katibu wa Chadema Kanda hiyo, Emmanuel Masonga na viongozi wengine.

Mbali na viongozi hao, pia maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wanapishana wodini hapo huku wakiendelea kuchukua taarifa muhimu kutoka kwa Mdude.

Habari zinazohusiana na hii

Akizungumza na Mwananchi Masonga amesema, “Bado wanaendelea na matibabu. Kwa sasa anachukuliwa vipimo vyote muhimu hivyo tunasubiri madaktari watatuambia nini. Na baada ya hapa tutakuwa mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia suala zima juu ya hili.”

Taarifa za kupatikana kwa Mdude eneo la Inyala, ziliaanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadaye kuwekwa wazi na diwani wa Kata ya Nsalala katika mji mdogo wa Mbalizi, Kisman Mwangomale.

Mwangomale amesema alipigiwa na simu na watu wa Inyala akijulishwa kwamba Mdude amepatikana huko na kwa muda huo alikuwa ofisi ya Serikali ya kijiji cha Inyala na kwamba walimtambua kuwa ndiye Mdude.

“Baada ya kupigiwa simu kuambiwa hivyo, nikaanza kuwapigia simu viongozi wangu (Chadema) wa juu lakini bahati mbaya walikuwa hawapokei simu.”

“Nikaona njia rahisi kuwafikia taarifa ili watume watu kwenda eneo la tukio ni kuandika kwenye makundi ya Whatsapp na imesaidia sana. Viongozi walichukua hatua ya haraka kwenda kumchukua na kumpeleka Hospitali,” amesema Mwangomale.



Chanzo: mwananchi.co.tz