Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa kata mbaroni kwa kumtandika makonde raia

Mbaroni Viongozi wa kata mbaroni kwa kumtandika makonde raia

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mbeya wanawashikilia Viongozi wawili wa Kata ya Iganzo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na Mwananchi mmoja kwa tuhuma za kumshambulia Kijana mmoja kwa kumtandika makonde ndani ya Ofisi ya Serikali.

Viongozi wanaoshikiliwa ni Diwani wa Kata hiyo, Daniel William (35), Ofisa Mtendaji wa Kata ya Iganzo, Erasto Mwankenja (48) na Mzee Henje Mbombo (74) ambaye ni Mwananchi wa kawaida wa Kata hiyo.

Polisi wamesema wamechukua hatua hiyo baada ya kusambaa kwa video ikionesha Viongozi hao wakimshambulia Kijana aitwaye Shadrack Zackaria (28) ambaye ni mpiga picha wa mtaani katika Kata hiyo ya Iganzo.

RPC wa Mbeya, Ulrich Matei amesema tukio la Viongozi hao kumshambulia kijana huyo limetokea March 03 mwaka huu katika Ofisi ya Kata hiyo iliyopo Mtaa wa Igodima "Chanzo cha tukio hilo ni Viongozi hao kumtuhumu Kijana huyo kuwapiga picha bila ridhaa yao wakati wakifanya shughuli za maendeleo na kudai Kijana huyo amewatolea lugha ya matusi wakati akiwapiga picha"

“Mama mzazi wa Kijana huyo ambaye anaitwa Esther Andrew aliziba njia iliyokuwa inakatisha kwenye shamba lake na ndipo Vionvozi hao wakaamua kuifungua na kulima barabara, sasa wakati wanaendelea na shughuli hiyo ndipo kijana huyo aliamua kuwapiga picha, Mama mzazi wa Zacharia ambaye ndiye mmiliki wa eneo ilipopitishwa barabara amesema alikuwa hajui kwamba mwanaye alishambuliwa, amesema alipata taarifa kwamba Mtoto wake huyo alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mbeya na amefanya taratibu zote za kumtoa bila kujua kwamba amekuwa ameshambuliwa na viongozi hao"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live