Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi ACT Wazalendo, mwandishi wa habari wapewa dhamana

73054 Pic+huru

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi watatu wa chama upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania na mwandishi wa habari mmoja waliokuwa wanashikiliwa na polisi nchini humo wamepata dhamana.

Waliokuwa wanashikiliwa ni pamoja na Mbarala Maharagande Katibu wa uadilifu, Mwikizu Mayama Mwenyekiti wa jimbo la Ilala, Haruna Mapunda mwandishi wa Gillybon na Saidi Mohammed Mwenyekiti wa Temeke.

Viongozi hao walikamatwa Jumamosi iliyopita Agosti 24, 2019 na jeshi la polisi wakati wakijiandaa kufanya mkutano wa ndani wa chama hicho Wilaya ya Temeke Dar es Salaam sambamba na ufunguzi wa matawi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Agosti 26, 2019 Wakili Bonifasia Mapunda amesema jeshi la polisi limewapa dhamana na kuwataka kuripoti tena kituoni hapo kesho asubuhi.

"Polisi wamekubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kuwataka kuripoti kituo cha polisi Chang'ombe kesho asubuhi ili kujua kama watafikishwa Mahakamani au la" amesema Wakili Mapunda.

Mkutano huo kabla ya kuzuiwa na kuamriwa kuondoka katika ofisi za chama hicho uliudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mshauri Mkuu wa ACT Maalim, Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dorothy Semi.

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz