Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana wawili mbaroni uvumi afya za viongozi

042329d059ada6eb473a755c11327029.jpeg Vijana wawili mbaroni uvumi afya za viongozi

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

POLISI mkoani Kilimanjaro imewakamata watu wawili kwa tuhuma za kusambaza uvumi katika mitandao ya kijamii kuhusu afya za viongozi wakuu wa nchi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alisema jana mjini Moshi kuwa watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti Machi 14, mwaka huu katika wilaya za Rombo na Moshi.

Makona aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Peter Pius (30) mkazi wa Tegeta mkoani Dar es Salaam, na Melchiory Slayo (36) mkazi wa Keni wilayani Rombo.

“Tumewashikilia watu hao kwa kosa la kimtandao ambapo walieneza uvumi wa viongozi wetu wakuu kuugua mmoja ambaye ni Silayo tulimkamata eneo la Kibaoni Tarakea Wilaya ya Rombo na Peter tulimkamata hapa Moshi Mjini,” Makona aliwaeleza waandishi wa habari.

Aliongeza, “wamefanya kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kwenye mitandao ya kijamii kinyume na Sheria ya Makosa ya Kimtandao kuwa viongozi wakuu wa serikali ni wagonjwa.”

Aidha, alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika ili sheria ifuate mkondo wake na iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika ametoa au amesambaza taarifa za kupotosha umma na kusababisha taharuki kwa jamii,” alisema Kaimu Kamanda.

Chanzo: www.habarileo.co.tz