Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana mbaroni kwa kukutwa na dola feki

Mwanamke Wa Afrika Kusini Alipatikana Na Hatia Ya Kuiba Dola Milioni 28 Vijana mbaroni kwa kukutwa na dola feki

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu Mkoani Njombe wanashikiliwa na Polisi baada ya kukamatwa na noti bandia 41 za kimarekani wakati wakienda kubadilisha katika benki ya NMB.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Hassan Banga amesema Vijana hao ni Stanley Menda (23), Priva Mbina (23) pamoja na Asia Kigoda (24) Wakazi wa Kibena Halmashauri ya Mji wa Njombe ambao wamekutwa wakiwa na noti bandia za Kimarekani (USD) 4100 sawa sawa na Tsh. 10,270,500.

“Wamekamatwa na noti 41 za kimarekani ambazo ni bandia, kati ya hizo nne walikuwa wanaenda kubadilisha katika benki ya NMB lakini 37 tumewakamata nazo nyumbani kwa hiyo upelelezi ukikamilika tutawafikisha Mahakamani”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live