Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo wawili wa halmashauri mbaroni

15146 Pic+vigogoo TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nyan’gwale. Vigogo wawili wa halmashauri ya wilaya ya Nyan’gwale mkoani Geita wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano ya upotevu wa Sh2 bilioni ambazo ni fedha za miradi ya maendeleo.

Vigogo waliokamatwa ni aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Carlos Gwamagobe na mtunza hazina wa halmashauri hiyo, Donatus Pangani wanaotuhumiwa kupora fedha hizo zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.

Miradi ambayo fedha zake hazionekani ni pamoja na fedha za mradi wa ujenzi wa jengo la halmashauri zaidi ya Sh900 milioni, fedha za mpango wa malipo kwa utendaji (P4R) zaidi ya Sh500 milioni na fedha za mradi wa kuboresha kituo cha afya Nyan’gwale zaidi ya Sh390 milioni.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Geita, Daniel Shila amekiri kushikiliwa kwa vigogo hao kwa ajili ya mahojiano lakini hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa kile alichodai kinaweza kuharibu uchunguzi.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, Hamimu Gwiyama amesema kukamatwa kwa vigogo hao kumetokana na taarifa ya makabidhiano ya ofisi kati ya mkurugenzi wa zamani na aliyeingia kupishana na taarifa za fedha zilizopo benki na hata alipotakiwa kutoa maelezo ameshindwa kuonyesha zilipo fedha hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz