Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo wa madini kuendelea kusota gerezani

43704 Pic+madin Vigogo wa madini kuendelea kusota gerezani

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) Archard Kalugendo na Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu, ambao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wakili wa Serikali, Salum Msemo amedai leo Jumatatu Februari 25, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaid kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini  upelelezi haujakamilika.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedai Wakili Msemo

Baada ya maelezo hayo hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 11,2019 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na kesi ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana.

Kalugendo na Rweyemamu ambao ni watumishi kutoka wizara ya madini, kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo, Septemba 15, 2017, wakikabiliwa na  shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.4bilioni.

Katika hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na mkoani Shinyanga.

Kwa pamoja wakiwa wathaminishaji almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara ya nishati na madini, waliisababishia Serikali hasara ya Dola 1,118,291.43 ambazo ni sawa na Sh2.4 bilioni.



Chanzo: mwananchi.co.tz