Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo UDA waendelea kusota rumande

HUKUMU Vigogo UDA waendelea kusota rumande

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema bado inaendelea na upelelezi katika kesi ya uhujumu inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Simon Bulenganija na wenzake wawili.

Mbali na Bulenganija, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 29/2023 ni Leonard Lubuye na William Kisena (44), wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kughushi mkataba wa kukodisha eneo la UDA kwa Kampuni ya Simon Group Limited na kuisababishia hasara shirika hilo, kiasi cha Sh14 bilioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Fatuma Waziri akisaidiana na Veronika Chimwanda, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, leo Novemba 13, 2023 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Waziri ameieleza Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, alidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake unaendelea hivyo, wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

"Shauri hili limeitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado unaendelea, hivyo tunaiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika," Amedai Waziri.

Hakimu Ruboroga baada ya kusikikiza maelezo hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 27, 2023.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kughushi mkataba wa kukodisha eneo la UDA lenye ukubwa wa ekari 13 lililopo Kurasini kwa Kampuni ya Simon Group Limited kwa gharama ya Sh400 milioni kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka 10, wakati akijua hati hiyo ya mkataba ni ya uongo.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kughushi mkataba wa kukodisha eneo tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Mei Mosi, 2011 na Desemba 31, 2018 katika Jiji la Dar es Salaam.

Siku hiyo, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kughushi mkataba wa kukodisha eneo la Uda lenye ukubwa wa ekari 13 lililopo Kurasini kwa Kampuni ya Simon Group Limited kwa gharama ya Sh400 milioni kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka 10, wakati akijua hati hiyo ya mkataba ni ya uongo.

Pia, wanadaiwa kutakatisha fedha, tukio analodaiwa kulifanya Desemba 31, 2018 katika jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, mshtakiwa alijipatia Sh14, 088, 983, 873 kutoka Shirika la UDA wakati akijua fedha hizo zinatokana na kosa tangulizi la kughushi.

Shtaka la tatu, ni kuisababishia hasara shirika hilo, tukio analodaiwa kulitenda kati ya Mei Mosi 2011 na Desemba 12, 2018 jiji Dar es Salaam, ambapo kwa makusudi na nia ovu alijipatia fedha Sh14 bilioni na hivyo kupelekee kulisababishia hasara Shirika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live