Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Serikalini waitwa kortini kesi ya mzee aliyepotea Loliondo

Hukumu Pc Data Vigogo Serikalini waitwa kortini kesi ya mzee aliyepotea Loliondo

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya kulazimishwa kupotea Oriais Oleng’iyo (85), mkazi wa kijiji Cha Ololosokwani kilichopo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, leo Machi 22, 2023 imekwama kuanza katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha baada wajibu maombi kutofika Mahakamani.

Kesi hiyo namba 68/2022 iliyofunguliwa na familia ya Oleng’iyo ilikuwa imepangwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji Mohamed Gwae.

Hata hivyo wajibu maombi kwenye shauri hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mkuu wa mkoa wa Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Arusha, mkuu wa wilaya ya Ngorongoro na mkuu wa polisi wilaya ya Ngorongoro, hawakufika Mahakamani.

Jaji Gwae amewataka wajibu maombi kufika Mahakamani huku akiwaagiza mawakili wa waleta maombi, Joseph Ole Shangai kutoka Kituo cha sheria na Haki za Binaadamu (LHRC), William Ernest na Simon Mbwambo kwenda na mteja wao ambaye ni mtoto wa mzee huyo anayedaiwa kutoonekana.

Jaji Gwae aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 30, 2023 kwa ajili ya kusikilizwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama, Wakili Ole Shanghai amesema walitegemea wajibu maombi kufika mahakamani kwa sababu tayari waliwapelekea hati ya mashitaka.

Hata hivyo, amesema wana imani Machi 30, 2023 watafika na wao watakuwa na mteja wao kama ambavyo Mahakama imeagiza.

Tangu kukamatwa kwa wananchi wapatao 19 wa loliliondo ambapo wengine walishafikishwa mahakamani na kesi yao kufutwa, Mzee Oleng’iyo inadaiwa ajulikani alipo.

Upande wa waleta maombi wanaiomba Mahakama hiyo iamuru wajibu maombi kumleta Mahakamani Oleng’iyo ambaye amepelekwa kusikojulikana tangu alipokamatwa nyumbani kwake Engong’u Nairowa, kata ya Ololosokwan, huko Loliondo wilayani Ngorongoro.

Pia, wameiomba Mahakama iamuru au kuwaelekeza wajibu maombi kumwachia huru Oriasi Pasilange Ng’iyo Kurosawa alikoshikiliwa tangu Juni 10, 2022 na iamuru walalamikiwa waje mahakamani kueleza sababu za kumshikilia Oriasi Pasilange Ng’iyo kinyume cha Sheria.

Katika ombi lingine wanaiomba mahakama iamuru na kuelekeza wajibu maombi kuleta mwili wa Oriaisi Ng’iyo akiwa hai au asipokuwa hai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live