Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Bodi ya Mkonge Tanga watupwa jela

Jela Pic Data Vigogo Bodi ya Mkonge Tanga watupwa jela

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Septemba 13, 2022 iliwahukumu Shabani Mapinda aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi na Imani Mduruma aliyekuwa Meneja wa Bodi ya Mkonge Nchini kifungo cha mwaka mmoja jela kwa matumizi mabaya ya Mamlaka.

Katika Shauri la Uhujumu Uchumi Namba ECC 06/2022, washtakiwa walipatikana na hatia ya kufanya uhamishaji wa shamba lililokuwa la Bodi ya Mkonge ( Farm no. 733/2) lililopo eneo la Hale wilayani Korogwe, kwenda kwa Kampuni ya HBU Katani Limited bila ya kuishirikisha Bodi ya Wakurugenzi.

Kila mshtakiwa ametakiwa kutumikia kifungo cha Mwaka Mmoja jela huku shamba hilo likiamriwa kurudishwa kwa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live