Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video za Sabaya akipewa mamilioni benki zaoneshwa Mahakamani

11f097586a18ac7395faee11d3570c7a.jpeg Video za benki zaoneshwa mahakamani kesi ya Sabaya

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha jana imetupa pingamizi lililowekwa na mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake sita.

Mahakama hiyo pia ilizipokea baadhi ya nyaraka kuwa vielelezo katika kesi hiyo zikiwemo video sita zilizorekodiwa benki ili zitumike kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.

Waendesha mashitaka waandamizi wa serikali wakiongozwa na Felix Kwetukia walimwomba shahidi wa nane, Johnson Kisaka (35) azioneshe video hizo mahakamani.

Kisaka ni ofisa uchunguzi katika maabara ya kiuchunguzi ya kielektroniki ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) jijini Dar es Salaam.

Alidai kuwa video hizo ni moja ya taarifa yake ya kiuchunguzi aliyoipata katika kamera za CCTV za Benki ya CRDB, tawi la Kwa Mrombo jijini Arusha.

Shahidi Kisaka alidai kuwa taarifa hiyo aliiandaa Mei 31 mwaka huu kuhusu tukio la Januari 22 mwaka huu.

Picha hizo za video zilionesha mtu mzima akiwakabidhi vijana wawili mamilioni ya fedha na kijana mwingine alikuwa nje akifuatilia ulinzi.

Nyaraka zingine zilizopokelewa kama ushahidi katika kesi hiyo ni fomu namba 28 ya taarifa ya kiuchunguzi kutoka kwa wataalamu wa IT wa benki ya CRDB na fomu namba 29 kuhusu taarifa ya Takukuru iliyokuwa ikieleza namna walivyofanya uchunguzi katika benki hiyo na kutoa taafa katika fomu hiyo.

Awali Hakimu Patricia Kisinda alisema mahakama imetupa pingamzi la mawakili wa utetezi kwa kuzingatia kifungua cha sheria ya ushahidi kifungu cha 64 (a) ya mwaka 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live