Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wanandoa matatani kwa upotoshaji kuhusu corona

VIDEO: Wanandoa matatani kwa upotoshaji kuhusu corona

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo linawashikilia wanandoa wawili kwa tuhuma za kusambaza taarifa za upotoshaji kwenye jamii kuhusu ugonjwa wa mlipuko wa virusi vya corona.

Kamanda Mambosasa ameeleza hayo mbele ya wanahabari leo Ijumaa Machi 27, 2020 wakati akizungumza masuala mbalimbali ikiwemo namna jeshi hilo linavyopambana kudhibiti uhalifu kwenye kanda hiyo.

Kamanda Mambosasa amesema wanandoa hao wakazi wa Tabata,  wanadaiwa kutoa taarifa hizo Machi 20  saa saba mchana wakiwa ndani ya daladala wakitokea Tabata kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akisimulia ilivyokuwa Kamanda Mambosasa amesema  wanandoa hao wakiwa katika daladala walisema "Serikali  inapotosha wananchi kwamba kuna virusi  vya corona na pia Serikali haina fedha za kulisha wanafunzi ndio maana shule na vyuo vimefungwa kwa kisingizio cha ugonjwa huo.

"Pia Serikali haina fedha kwa hiyo inataka msaada kutoka mataifa ya nje. Baada ya abiria kusikiliza uzushi na upotoshaji huo wakamuelekeza dereva kupeleka gari kituo cha polisi cha kati na watuhumiwa walishikiliwa," amesema Kamanda Mambosasa.

 

Pia Soma

Advertisement
Kamanda Mambosasa amesema upelelezi wa shauri hilo umekamilika na jalada lipo kwa mwanasheria wa Serikali  na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

Mbali na hilo, Kamanda Mambosasa amesema jeshi hilo linawashikilia watu watano kwa kufanya uhalifu kwa kutumia silaha za jadi ikiwemo mapanga, marungu.

Alisema wkamba Machi 22 watu hao walimvamia ofisa wa Serikali  Victor Nyirenda na kumjeruhi kichwani kisha kumpora simu mbili, kompyuta mpakato, pochi pamoja na fedha Sh500,000.

"Kwa ujumla walifanya uporaji wenye thamani ya zaidi ya Sh3 milioni. Baada ya kufanya tukio hili polisi kikosi malaumu kilianza ufuatiliaji na kuwakamata watuhumiwa wote," amesema Kamanda Mambosasa.

Mbali na hilo, Kamanda Mambosasa pia alisema polisi ilifanya upekuzi kwenye maduka ya watuhumiwa wanakopeleka vitu vya wizi na kukamata kompyuta mpakato 34, simu 10, luninga, deki na chaji za kompyuta.

Chanzo: mwananchi.co.tz