Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wabunge Chadema wasomewa mashtaka saba

Video Archive
Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wabunge watatu wa Chadema, Halima Mdee, Ester Bulaya na Jesca Kishoa pamoja na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo Jumatatu Machi 23, 2020 na kusomewa mashtaka saba.

Kati ya mashtaka hayo yapo ya kuharibu geti kuu la mlango wa kuingilia gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, kutotii amri halali na kutoa lugha ya kuudhi  kwa askari wa Jeshi la Magereza.

Wamesomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na  jopo la mawakili watatu wakiongozwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Renatus Mkude. Wengine ni Mkunde Mshanga na Ester Martine.

Wakili Mkude amedai  washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa yao Machi 13, 2020 katika gereza la Segerea Wilaya ya Ilala.



Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz